View profile

Jarida La Ujasusi - Issue #1

Ujasusi
*********************Kwanini ujiunge na jarida hili**********************

Kwanza, hili ni jarida la kwanza DUNIANI katika lugha ya Kiswahili linalohusu habari za intelijensia hususan ujasusi na usalama wa mtandaoni hususan udukuzi. Endapo maneno “intelijensia” na “ujasusi” yanakuchanganya, kwa kifupi ni kwamba “ujasusi” ni moja ya vipengele katika taaluma ya “intelijensia.” Hata hivyo mara nyingi “ujasusi” hutumika kumaanisha “intelijensia” au kinyume japo si sahihi. Pengine hiyo ni kutokana na ukweli kwamba neno “jasusi” (kwa kimombo “spy”) ni maarufu zaidi kuliko “intelijensia” (kwa kimombo “intelligence’)
Pili, mwanzilishi na mwendeshaji wa jarida hili ni mtu mwenye ujuzi wa taaluma zote mbili zinazohusiana na jarida hili, yaani intelijensia na usalama wa mtandaoni. Aliwahi kuwa mwana-intelijensia nchini Tanzania kwa miaka kadhaa na kwa sasa ni msadi katika usalama wa mtandaoni akijihusisha na udukuzi wa kimaandili (kwa kimombo "ethical hacking”)
Tatu, malengo makuu mawili ya jarida hili ni KUHABARISHA na KUELIMISHA. Kwa maana hiyo, kwa kununua jarida hili sio tu utahabarika kuhusu intelijensia na usalama wa mtandaoni bali pia utapata fursa adimu ya kujifunza maeneo mbalimbali muhimu yanayohusiana na taaluma hizi nyeti. Bila shaka ungependa kujifunza japo kidogo kuhusu udakuzi wa kimaadili. Basi umefika mahala stahili kwani kuna darasa litakalokujia kuhusu somo hilo.
Nne, gharama ni nafuu. Kwa mwezi ni USD 5 (takriban sh 11,500 hivi) ambapo utapokea matoleo manne au matano kutegemea urefu wa mwezi.
Waweza kulipia kwa TZS kwa kubonyeza HAPA.
Karibu sana
Don’t miss out on the other issues by Evarist Chahali
Did you enjoy this issue? Yes No
Evarist Chahali
Evarist Chahali @chahali

News and commentary on intelligence, espionage, spies, spying, hackers and hacking. Ujasusi means espionage in Swahili

You can manage your subscription here.
In order to unsubscribe, click here.
If you were forwarded this newsletter and you like it, you can subscribe here.
Created with Revue by Twitter.