Ujasusi

By Evarist Chahali

Jarida La Ujasusi - Toleo Maalum (La Bure) Kuadhimisha Kipigo Cha Bashite: Tafsiri Ya Kijasusi Ya Tukio Hilo La Kihistoria

#8・

Stay up to date, be part of a community and show your support.

81

issues

Ujasusi
Jana ilikuwa siku njema sana baada ya mwanasiasa ambaye yayumkinika kumtaja kama “mtu anayechukiwa zaidi kuliko Mtanzania mwingine yeyote yule,” Albert Bashite, alipoangushwa katika kinyang'anyiri cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Kigamboni.
Evarist Chahali
Hate figure: yayumkinika kusema Bashite ndo mtu anayeongoza kwa kuchukiwa Tanzania. Na huenda hajawahi kutokea Mtanzania aliyewahi kuchukiwa kiasi hiki. https://t.co/1EWdQWhfCV
Nikiri kwamba awali niliona kama jambo lisilowezekana kwa Bashite kuangushwa huko Kigamboni, kwa sababu kadhaa. Moja ni ukweli kwamba kulikuwa na hisia kwamba wazo hilo la Bashite kugombea ubunge Kigamboni lilikuwa na baraka za “baba yake” Magufuli.
Evarist Chahali
Namchukia Bashite kwa nguvu zangu zote lakini unfortunately sioni mwenye jeuri ya kumkata huko Kigamboni. Uamuzi wake wa kutangaza nia una baraka za baba yake @MagufuliJP ambaye sasa hivi ameiweka CCM mfukoni https://t.co/cgFdeSmBuw
Lakini pengine kubwa zaidi ni tetesi za kijasusi kuhusu uwepo wa mkakati wa Magufuli kuliweka bunge mfukoni kwa kumpatia Uspika Bashite.
Evarist Chahali
Safari ya Bashite kuelekea Uspika katika bunge lijalo imeanza rasmi. Asubuhi kachukua fomu, jioni baba yake - @MagufuliJP - kalazimika kutangaza teuzi nyiiiingi kuficha ukweli kuwa motive ilikuwa kumpumzisha mwanae ajiandae kushinda jimbo Kigamboni kisha awe Spika #MarkThisTweet https://t.co/qvqS1TnG8f
Evarist Chahali
Tetesi zinadai kuwa endapo yule mtu mfupi ataondoka, basi Magufuli atamteua Bashite kuwa mbunge kisha kufanya uchakachuzi utakaomwezesha DAB kuwa Spika. https://t.co/ffbDIhBEo6
Lakini jingine lililofanya watu wengi waamini kuwa Bashite angeshinda jana ni ukweli kwamba mpinzani wake mkuu alikuwa Dkt Faustine Ndugulile, ambaye licha ya kuwa mbunge wa sasa wa jimbo hilo aliishia kuondolewa madarakani kwa uonevu na Magufuli.
Consumer Grassroots
Tanzania President John Pombe Magufuli has fired the deputy Minister of Health Faustine Ndugulile for 'not cooperating' in managing the coronavirus pandemic. #covid19Tanzania https://t.co/seQh7bgsSU
Lakini licha ya kuweka hayo yote, Bashite alijijengea umaarufu kama mtu ambaye ana jeuri ya kufanya lolote bila kuhifia kuchukuliwa hatua na Magufuli.
Kuna Siri Gani Kati ya Magufuli Na Daudi Albert Bashite? | by Evarist Chahali | Medium
Na licha ya matukio mbalimbali aliyofanya Bashite ikiwa ni pamoja na lile la uvamizi Clouds FM, bado hakukuwa na dalili za Magufuli kumchukulia hatua Bashite.
Namna Makonda alivyo vamia Clouds fm na POLISI
Namna Makonda alivyo vamia Clouds fm na POLISI
Na akafanya kebehi hadharani pale alipokosolewa
Dharau za Bashite
Dharau za Bashite
Kwahiyo kulikuwa na kila sababu ya kuhisi kuwa Bashite angeibuka kidedea jana. Lakini haikuwa hivyo.
Kwanini ameanguka?
Jibu la wazi ni kwamba “baba yake (Magufuli) amemtelekeza.” Kwanini amemtelekeza? Hilo lahitaji kuchimba kwa undani kabla ya kukurupuka na majibu ya mhemko.
Kwa maana laiti Magufuli angeamua kumbeba Bashite, ni wazi angewatumia “mabingwa na sanaa za kiza” (dark arts), Idara ya Usalama wa Taifa, kumsaidia kushinda uchaguzi hu.
Na kuashiria kuwa Bashite anachukiwa, jana nilipata salamu kutoka kwa marafiki wa zamani huko “Kitengoni” wakinijulisha kuwa Bashite kaangushwa.
Je licha ya kuwa jambo la kupendeza, kuangushwa huko kuna faida yoyote ya muhimu?
Kwa juu juu, anguko hilo la Bashite jana linakidhi tu kiu ya watu wengi kumuona akupata machungu kama alivyosababisha machungu kwa watu wengi.
Lakini anguko hilo pia linatoa picha pana zaidi. Kilichomfanya Bashite aanguke jana ni kwamba wana-Kigamboni waliamua “liwalo na liwe.”
Hata hivyo, picha kubwa zaidi ni kwamba WATANZANIA WAKIAMUA WANAWEZA. Kwamba kama chuki yao dhidi ya Bashite imeweza kumnyima kura, ni wazi basi chuki hiyo ikielekezwa kwenye utawala kandamizi wa Magufuli inaweza pia kumnyima sapoti.
Ofkoz kwa upande wa Magufuli kunahitajika factors nyingine (mfano sapoti ya Kitengo) ku-remain constant, lakini ni mahala pazuri kuanzisha chachu ya mabadiliko.
Je anguko la Bashite linaweza kuamsha ari ya mabadiliko?
Watanzania wana kiu ya mabadiliko lakini wanakosa uongozi wa harakati za mabadiliko hayo. Vyama vikuu vya upinzani vipo bize zaidi na malalamiko kuwa wanaonewa badala ya kufanya jitihada za kuhamaisha umma kukomesha uonevu huo. Malalamiko pekee hayawezi kuung'oa utawala kandamizi.
Je anguko la Bashite jana ndio mwisho wake?
Inategemea jinsi atakavyocheza karata zake baada ya anguko hilo la jana. Kwamba Magufuli anaweza kuamuru vikao vya CCM vipitishe jina la Bashite, kwa sasa inaonekana ni jambo lenye uwezekano mdogo. Hata hivyo, ni kosa kum-underestimate adui. Yayumkinika kuhisi kuwa Bashite anaweza kufanya lobbying na akafanikiwa kurudi kwenye nafasi za uongozi. Ni muhimu kuuacha muda uongee.
Endeleo kupata habari na elimu mbalimbali katika jarida hili la ujasusi.
MATANGAZO
Huduma za usadi wa siasa (political consulting)
Vitabu Vya Chahali
Flutterwave - Evarist Chahali
Don’t miss out on the other issues by Evarist Chahali
Did you enjoy this issue? Yes No
Evarist Chahali
Evarist Chahali @chahali

News and commentary on intelligence, espionage, spies, spying, hackers and hacking. Ujasusi means espionage in Swahili

You can manage your subscription here.
In order to unsubscribe, click here.
If you were forwarded this newsletter and you like it, you can subscribe here.
Created with Revue by Twitter.