Ujasusi

By Evarist Chahali

Jarida La Ujasusi - Toleo La Pili: Dondoo 8 Muhimu Za Kijasusi Zinazoweza Kukuokoa Katika Zama Hizi za #WatuWasiojulikana.'

#2・

Stay up to date, be part of a community and show your support.

81

issues

Ujasusi
Dondoo 8 Muhimu Za Kijasusi Zinazoweza Kukuokoa Katika Zama Hizi za ‘Watu Wasiojulikana.’

Tanzania inapitia katika nyakati hatari ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya watukuchukuliwa na “watu wasiojulikana.” Japo kundi hilo la “watu wasiojulikana” halifahamiki (na ndio maana linaitwa hivyo) takriban mara zote limekuwa likitumia mbinu zinazoshabihiana, ambapo kuna dalili japo kidogo za ujasusi. Ni kwa mantiki hiyo, makala hii fupi inakueleza mbinu 8 muhimu zinazoweza kukusaidia kujikinga dhidi ya kundi hilo hatari
Huenda unajiuliza, kwani kuna tofauti kati ya JASUSI na AFISA USALAMA WA TAIFA (aka SHUSHUSHU)? Jawabu ni kwamba UAFISA USALAMA WA TAIFA ni taaluma ya jumla katika namna ilivyo kwenye uhandisi au udaktari au uanahabari. Kwa mfano, kwenye uhandisi kuna wahandisi wa ujenzi, uhandisi wa kemia, nk ilhali kwenye udaktari nako kuna udaktari wa magonjwa ya moyo, udaktari wa maradhi ya akina mama, nk na kwenye uanahabari kuna waandishi wa habari (wanaotafuta na kuchapisha habari), watangazaji wa redio, watangazaji wa runinga, nk
Na kwenye UAFISA USALAMA WA TAIFA kuna mashushushu wanaofanya kazi ndani ya nchi ambao ni asilimia kubwa zaidi. Na pia kuna wanaohusika na ulinzi wa viongozi (baadhi yao huonekana wameambatana na viongozi japo kuna idadi kubwa zaidi ya “wasioonekana”) na kuna wanaofanya kazi nje ya nchi aidha kwa uwazi kidogo (kama maafisa ubalozi) na kwa usiri mkubwa. Hawa ndio MAJASUSI. Ujasusi ni kufanya ushushushu nje ya nchi. Ni kazi ya hatari mno.
Hata hivyo, baadhi ya mashushushu wa ndani hutumwa nje kufanya ujasusi na wakirudi nyumbani wanaendelea na ujasusi wa ndani. Kadhalika, kwa vile kila nchi inafanya ujasusi dhidi ya nchi nyingine, kila nchi nayo inapaswa kuwa na mashushushu wanaokabili ujasusi kutoka nje, neno la kimombo ni “counterespionage.” Wakati mwingine neno linalotumika ni “counterintelligence” linalomaanisha mashushushu waliopo ndani ya nchi wanaokabiliana na mashushushu kutoka nje ya nchi.
Nihitimishe kwa kukuhakikishia kuwa kamwe hutojilaumu kununua jarida hili ambapo sio tu utapata uelewa kuhusu masuala mbalimbali lakini pia utaweza kujibiwa maswali kadhaa unayoweza kuwa nayo kuhusu intelijensia, ujasusi, na udukuzi kwenye usalama wa mtandaoni. Pia jarida hili litakuwa linakupatia kozi mbalimbali za bure sambamba na vitabu vinavyohusiana na kozi hizo pamoja na apps muhimu kwa simu au kompyuta yako.
Fanya pia kumjulisha ndugu, jamaa na rafiki kuhusu jarida hili.
Katikati ya Ishu za Ujasusi na Udukuzi, Dozi ya 'Jinsi ya Kuwa Mtu Bora' (Personal Development) Yaweza Kuwa Muhimu
Baada ya miaka takriban 20 hivi ya kuongelea ishu za siasa, mwaka juzi niliamua kujiweka kando kidogo na masuala ya siasa na kuwekeza nguvu zaidi kwenye taaluma ya intelijensia ambayo nafanyia usadi pia (angalia HAPA) sambamba na kujenga “mahaba mapya” kwenye “jinsi ya kuwa mtu bora” ambayo kwa kimombo inafahamika kama “personal development.”
Kadhalika, mwaka huo huo wa 2018 nilipewa ushauri ambao kwa hakika umeniongezea kitu kimoja muhimu sana maishani. Naamini watu wengi wanamkumbuka mwanahabari Eric Kabendera. Basi mwaka juzi alikuja UK kikazi, na katika maongezi yetu alinipa ushauri mmoja muhimu sana.
Alinambia kuwa kutokana na background yangu ya ujasusi, na kwa vile nimekuwa mwenye mahaba na masuala ya teknolojia, basi alidhani kuwa ndoa kati ya intelijensia na teknolojia ingeweza kunifanya mtu bora zaidi. In fact alichomekea, “unaweza kuwa #MtuHatari kwelikweli,” 😁
Na nikafanyia kazi ushauri wake. Nikawekeza nguvu kwenye kujielimisha masuala mbalimbali ya teknolojiia, nikafanya kozi ya udukuzi wa kimaadili, sambamba na kurukia takriban kila kozi niliyokutana nayo mtandaoni, na kwa sasa naweza kwa hakika kusema sio tu nimeingia rasmi kwenye fani hiyo bali pia nimepata uzoefu wa kutosha.
Kwahiyo, ukiweka kando mahaba yangu kwenye masuala ya intelijensia na teknolojia, suala la “jinsi ya kuwa mtu bora” limekuwa na kipaumbele kikubwa kwangu. Na tofauti na nilivyotengeneza maadui wengi kwenye masuala ya siasa, “jinsi ya kuwa mtu bora” imenijengea marafiki wengi, na nimeweza kuwasaidia watu wengi zaidi ya nilivyokuwa napiga makelele kwenye siasa.
Kwahiyo basi nitajitahidi katika kila toleo la jarida hili kuweka mada japo fupi ya “jinsi ya kuwa mtu bora.” Kadhalika, kama ishara ya kuthamini kujiunga na jarida hili, atakayenunua toleo moja la kitabu changu cha “Jinsi Ya Kuwa Mtu Bora” atapata toleo jingine bure. Yaani ukinunua toleo la kwanza, unapewa toleo la pili bure au kinyume chake. Na kama ni mvuta sigara, basi utapatiwa kitabu cha “Jinsi ya Kuacha Kuvuta Sigara” bure pia.
Duka la vitabu hivyo lipo hapa
Vitabu Vya Chahali
Na mada fupi kuhusu “jinsi ya kuwa mtu bora” katika toleo hili inahusu kutokata tamaa. Mara nyingi, na pengine mara zote, mwanzo huwa sio tu ni mgumu bali huambatana na maswali kama endapo jambo husika lina maana, sambamba na changamoto kutoka kwa watu waliotuzunguka.
Nakumbuka nilipochapisha kitabu changu cha kwanza kabisa, nidhihakiwa na watu flani mtandaoni kuwa “ah huyu yupo Ulaya anauza vitabu Tanzania, atakuwa na maisha magumu.” Kana kama ni dhambi kuwa na maisha magumu.
Lakini sikutoa fursa kwa kelele hizo hasi, nikaendelea na uandishi na hadi muda huu nimechapisha lundo la vitabu. Baadhi ya vitabu hivyo ni hivi hapa
Baadhi ya watu walionidhihaki mwanzoni waliishia kuwa mashabiki wa vitabu vyangu. Lakini hilo si muhimu zaidi ya ukweli kwamba uandishi wa vitabu umenitengenezea kitu muhimu maishani - kuwa moja ya vyanzo vya kuhabarisha na kuelimisha watu mbalimbali duniani.
Naam, mwanzo ni mgumu, lakini waweza kurahisisha ugumu kwa kujenga msingi mapema. Na msingi huo ni pamoja na kujiuliza mapema kwanini unataka kufanya kitu flani. Si kila tufanyacho lazima kiwe na thamani in terms of fedha. Kwa mfano japo jarida hili sio la bure, lakini lengo si kupata fedha bali kuhabarisha na kuelimisha. Hata hivyo, pesa itakayopatikana kwenye mauzo ya jarida hili itasaidia sio tu kuliboresha lakini pia kunipatia motisha.
Hebu angalia video hii fupi. Kisha tafakari.
Naam, kuna nyakati utaanza na kulazimika kusimama, kwa muda mfupi au kwa muda mrefu. Kusimama huko hakupaswi kuwa mwisho wa kitu hicho unless unabaini hakina tija. Uzoefu waonyesha kuwa vitu vinavyotengenezeka haraka havidumu. Ni kama umaarufu unaokuja ghafla, ni nadra kudumu. Wako wapi akina “Dokta Shika” au “Piere Likwidi”?
Kwahiyo naomba kutumia fursa hii kukumbushia umuhimu wa kutambua kuwa mara nyingi mwanzo ni mgumu lakini ugumu huo haumaanishi kuwa lengo kusudiwa halitofikiwa.
Kadhalika, ni muhimu kutambua kuwa stops katika safari ya kuelekea uendako hazimaanishi mwisho wa safari.
Na kelele au dhihaka dhidi ya unachoanza kukifanya ziwe kuni za kuchochoea dhamira yako badala ya kukuvnja moyo.
Hadi toleo jingine, ndimi kocha wako!
Kozi Mbalimbali Za Bure Zinazohusiana na Usalama wa Mtandaoni na/au IT kwa ujumla
Learn how Domain Names Work and Types of Web Hosting for any Web Development Project
Learn how the Internet Works - HTTP/HTTPS, Mail Delivery (SMTP), LAN, WAN, Network Basics & Firewalls
Learn to Build Database Driven Web Applications using PHP & MySQL
Lean the Foundations of HTML & CSS to Create Fully Customized, Mobile Responsive Web Pages
Learn how to Add Dynamic Client-Side Functions to your Web Pages using CSS & JavaScript
Don’t miss out on the other issues by Evarist Chahali
Did you enjoy this issue? Yes No
Evarist Chahali
Evarist Chahali @chahali

News and commentary on intelligence, espionage, spies, spying, hackers and hacking. Ujasusi means espionage in Swahili

You can manage your subscription here.
In order to unsubscribe, click here.
If you were forwarded this newsletter and you like it, you can subscribe here.
Created with Revue by Twitter.